Naomba ushauri: Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 27 naishi Buza jijini Dar

Image may contain: 1 person
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 27 naishi Buza jijini Dar na nina mpenzi wangu ambaye amenisomesha toka form one hadi sasa nimemaliza chuo kwani wazazi wangu walifariki wakati mimi nikiwa mtoto mdogo sana.

Amenigharamia sana, kuanzia nguo hadi chakula ninacho kula vyote ni msaada wake yeye na amejitolea kuninunulia gari la kutembelea na kanambia nitafute kiwanja ili tujenge nyumba ya kupangisha.

Nimemaliza chuo mwaka huu mungu si athumani nimefaulu, ila naombeni ushauri jamani mimi simtaki tena nampenda kaka mmoja nimesoma nae chuo na tushaanza mahusiano, jamani nisaidieni nifanyaje??

Naombeni ushauri.

Comments