MWANAMKE / MAMA IJUE NAFASI YAKO ILI UWEZE KUSABABISHA USTAWI KATIKA FAMILIA YAKO.


Mumeo ni mtu ambaye hajakamilika hivyo usitarajie mengi kutoka kwake, wewe mama Mungu amekuumba ili kumkamilisha, wanawake wasiyo jua hili wakiolewa wanasababisha uharibifu mkubwa kwa waume zao na mwisho wanakuwa maskini lakini wale wanaojua kuwa wanaume hawajakamilika na wao wameolewa ili kuwakamilisha wanasababisha waume zao na familia kwa ujumla KUSTAWI.

Mwanaume anapata ujasiri wa kutafuta pesa akisifiwa na mkewake, hatarudi nyumbani mikono mitupu hivyo jifunze kumsifia mume wako.
Mwanamke au mama wa familia jitahidi kukaa kwenye nafasi yako ili uweze kuona furaha na Baraka za familia yako na wewe ambaye bado haujaolewa ukiyaelewa haya utasababisha yule aliyeumbwa kwa ajili yako atoke huko aliko akufuate.

Comments